Zlatan Ibrahimovic Kwenye Mikono Ya Sheria.

Maisha ya mchezaji sio tu uwanjani, yanahusisha mahusiano yake nje ya uwanja kwa kiasi kikubwa. Mchezaji wa AC Milan na timu ya Taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic, ameingia kwenye mikono ya sheria.

Ibrahimovic anafanyiwa uchunguzi na kamati ya maadili ya Uefa kwa kile kilichoripotiwa kuwa mchezaji huyo anajihusisha na masuala ya michezo ya kubashiri.

Kwa mujibu ya sheria za Uefa, ni marufuku kwa mchezaji yeyote kujihusisha na masuala ya kubashiri michezo. Zlatan Ibrahimovic, ametajwa kuingia ubia na kampuni inayojihusisha na michezo ya kubashiri na hivyo kuingia kwenye mikono ya sheria kwa kuvunja sheria za Uefa.

Taarifa ambayo imetolewa nchini Sweden kama ambavyo imechapishwa na Uefa imesema, ” Afisa ya upelelezi wa maadili na nidhamu wa Uefa, ameteuliwa leo kuanza uchunguzi wa kinidhamu kuhusu kuvunjwa kwa taratibu za kinidhamu za Uefa ambapo kumefanywa na Mr. Zlatan Ibrahimovic ambaye anahusishwa kuwa na ubia na kampuni ya kubashiri”

Lukaku (kushoto) akigombana na Zlatan (kulia)

Hii ni mara ya pili kwa Zlatan kuingia kwenye mikono ya sheria msimu huu. Itakumbukwa kwenye mchezo wa Coppa Italia dhidi ya Inter Milan, Zlatan aliingia kwenye ugomvi na Romelu Lukaku ambapo mzozo huo uliwafanya wote wawili kupigwa faini kwa kosa hilo.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

10 Komentara

    Zlatan ameshakuwa jipu Sasa uefa

    Jibu

    Pole sana.ibra

    Jibu

    Asamehewe tu

    Jibu

    Dah pole kwa ibra

    Jibu

    Dhuuu

    Jibu

    Ibra utoshek na mkwanja

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Duh pole yake

    Jibu

    Duuh Sio poa

    Jibu

    Haya majanga kwa Movic

    Jibu

Acha ujumbe