Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez, amefanikiwa kupata uteuzi kupitia shirikisho la mpira wa mguu barani Afrika CAF.

Barbara amechaguliwa kua makamu wa Rais wa  kamati ya mashindano inayosimamiwa na CAF, na usimamizi wa leseni za klabu katika mashindano yanayohusiana na shirikisho hilo linalosimamia mpira wa Afrika.

barbaraKiongozi huyo wa klabu ya Simba ataitumikia nafasi hiyo kwa muda wa miaka miwili ndani ya shirikisho hilo, kuanzia mwaka 2022 mpaka mwaka 2024 huku akiwa akitokea pekee kama mwanamke kwenye orodha hiyo huku Rais wake akiwa Ahmed Yahya katika majukumu yake.

Kiongozi huyo ambae amekua akifanya vizuri kwa mwaka wa tatu sasa katika klabu ya Simba, huku akiwa na mafanikio kadhaa ndani ya timu hiyo ikiwa kufanikisha timu hiyo kufika hatua ya Robo fainali ligi ya mabingwa Afrika pamoja na Robo fainali ya kombe la shirikisho Afrika.

Na kufanya vizuri na klabu ya Simba kumempa nafasi ya kuonekana na kupata nafasi kwqenye shirikisho la soka Afrika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa