Tunahitaji kuwa na Timu ya Taifa bora wakati tunasupport sera ya wachezaji 12 wakigeni kwenye Ligi ya Nchi tena ikiwezekana wapatikane wote Wenye Quality hasa kwenye best 11 ya vilabu venye sura ya mradi wa soka letu. sababu kuu ligi itakua na ushindani na Wachezaji wazawa watahamasika . hivi quality na Consistence vinapatikana tu bila ya kucheza kila Mara tena kwenye soka ushindani.( Vilabu)
Soka
Soka

Tunawashangaa Congo kuwaacha kina YANNICK NA FISTON ambao huku ndio wimbo wetu ndio Wenye soka letu , Bado tunaanzisha AGENDA SETTING kuhusu wao .hatujiulizi wao Wana Bidhaa ngapi nje ya soko lao.?

Soka linamuhitaji Binadamu ambaye atapitia kwenye UKUAJI ndipo baraka za kutosha zitatolewa kuelekee Kwenye USHINDANI .

Kama inapita miaka miwli… ndio tunatoa Bidhaa kwenda nnje tena ikapatiwe maboresho ya kutosha ,vipi hizi products nyengine zilizopo nyuma ya hio iliyotoka ?


Njia mbili tu kukuza (kuwekeza) Wenyewe au kutoa nnje .vipi lipi tunaliweza hapo?

Hapo kwenye Wenyewe nahisi tuna mlima mkubwa sana hadi tuupandishe na kufika kilele Cha ahadi tutakuwa tumeshachelewa na ndoto zetu huku mitaani zitakuwa zimejifia tayari. Academy nyingi zenye ubora ,Walimu Wenye uweledi Pamoja na uzoefu , miundombinu (ndio Baba wa sura zote za projects za kuwekeza ndani) , Mashuleni soka lipewe kipaombele (wasimamizi wa programs wawe na uweledi wa kutosha wafahamu vijana Tunahitaji nini) Serekali ijitoe kwenye Sector hii Kama huko kwenye utalii , kilimo n.k . nahisi mpaka hapo tu ushafahamu mlima wetu upo wapi.

 

Soka

 

Hapo kwenye kutoa nnje nahisi ndipo kwenye Uhai wetu kwasasa , natamani Taasisi Kama ya ziwe nyingi hapa kwetu ili vijana hata Senior wapate nafasi ya kwenda nnje kukua kisoka na wapate ushindani wa kutosha huko . ili wakirudi wawe imara Maana sisi nahisi tumemaliza mwendo .


Kwa habari na matukio ya kimichezo na ya uhakika tembelea Youtube channel yetu Meridian Sport


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa