Kinda wa Manchester United, Shola Shoretire, amesaini mkataba wake wa kwanza kama mchezaji wa kulipwa akiwa na United.

Shoretire amekuwa na wakati mzuri katika kikosi cha wachezaji vijana wa klabu hiyo (U23) msimu huu akiwa miongoni mwa wachezaji hatari zaidi kwenye Premier League 2.

Shola Shoretire ambaye pia ni raia wa Nigeria, alikataa kuungana vilabu vikubwa kama PSG, Barcelona, Juventus na Bayern Munich ili aendelee kuitumikia United.

Makali ya Shoretire yanaendelea kuchagizwa na ujio wa Amad Diallo ambapo wachezaji hawa wamekuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha timu hiyo katika michezo miwili waliyocheza pamoja.

Amad Diallo (kushoto) akiwa na Shoretire (kulia)

Kutokana na kiwango chake, kocha Ole Gunnar Solskjaer ameamua kumjumuisha Shoretire kwenye kikosi cha wachezaji wakubwa na ameanza kufanya nao mazoezi tangu Jumapili.

“Ndoto yangu ya kusaini mkataba wangu wa kwanza na timu ninayoishabikia tangu utotoni imetimia. Ni siku ya kujivunia kwangu na familia yangu.

“Ninawashukuru watu wote kwenye klabu na familia yangu kwa kuniwezesha kufikia wakati huu. Jitihada zinaendelea!” aliandika Shoretire kupitia ukurasa wake wa Instagram.


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBET 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa