Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Didier Gomes amesema kuwa hajui alipo mshambuliaji wake Lokosa Junior. Lokosa Junior raia wa Nigeria alisajiliwa na Simba kwa dili la miezi 6 na sababu kubwa ya usajili wake ni kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gomes

Akiwa ndani ya kikosi cha Simba hajaweza kuonekana kwenye mechi ya ushindani ambapo Simba ikiwa imecheza mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi hajacheza mchezo hata mmoja.

Nafasi yake ya ushambuliaji amekuwa akianza Chris Mugalu pamoja na Meddie Kagere ambaye mechi nyingi amekuwa akianzia benchi huku John Bocco taratibu akirejea kwenye ubora wake.

Gomes
Mugalu na Kagere

Katika mazoezi ya Simba ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Simba Mo Arena vilivyoppo Bunju, Lokosa hajaonekana mazoezini huku habari zikieleza kuwa amevunjiwa mkataba wake na mabosi hao wa mtaa wa Msimbazi.

Gomes

Kuhusu Lokosa, Gomes amesema:“Sijui kwa kweli kuhusu huyo, ila siwezi kulizungumzia jambo hilo ila ukweli ni kwamba sijamuona muda mrefu kwenye eneo la mazoezi,”.|


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Gomes, Sijui Lokosa Aliko – Gomes, Meridianbet

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa