Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemfungia mchezaji wa Simba SC, Ibrahim Ame Mohamed michezo mitatu na faini ya Sh500, 000 kwa kosa la kumzuia mwamuzi msaidizi wa mchezo kati ya Gwambina na Simba kufanya kazi yake.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatano Aprili 28, 2021 imesema kuwa adhabu hiyo imetolewa baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kukaa kikao chake cha Aprili 27, 2021 cha kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.

 

simba, Simba :Ame Afungiwa Mechi 3 na TPLB., Meridianbet

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, kosa la Ame alilifanya katika mchezo uliochezwa Aprili 24, 2021 kwenye uwanja wa Gwambina mkoani Mwanza.

“Mchezaji wa Simba SC Bw. Ibrahim Amme Mohamed amefungiwa michezo mitatu (3) na faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumzuia Mwamuzi msaidizi wa mchezo huo kufanya kazi yake” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 39:5(5.6) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa