Nyota watatu wa Simba SC wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao waliongia kwenye kinyang’anyiro hicho ni Clatous Chama, Aishi Manula na Shomari Kapombe ambao mmoja wao atashinda kutokana na idadi ya kura atakazopata.

Wachezaji watano waliingia kwenye kinyang’anyiro hicho lakini Kamati maalumu iliwachuja na kubaki na watatu ambao watapigiwa kura na mashabiki kupitia Tovuti rasmi ya klabu. Nyota wawili ambao walifika hatua hiyo ni Luis Miquissone na Pascal Wawa.

 

simba, Simba : Chama, Manula na Kapombe Nani Mchezaji Bora wa Mwezi., Meridianbet

Tuzo hii ambayo inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile itakuwa ni ya tatu kutolewa tangu ilipoanza mwezi Februari mwaka huu.

Mchezaji atakayepata kura nyingi atakabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium kushirikiana.

Miquissone alikuwa mchezaji wa kwanza wa Simba SC kutwaa tuzo hiyo mwezi Februari wakati Joash Onyango alishinda mwezi Machi.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa