Mwekezaji wa Simba, Mo Dewji amekiri kwamba kwa sasa timu hiyo ni moja kati ya timu kubwa sana barani Afrika. Simba imeingia kwenye robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika ikishinda mechi nne, kusulu moja na kupoteza moja na kumaliza kama kiongozi wa kundi B juu ya Al Ahly.

Simba wamekuwa na kipindi kizuri sana msimu hasa kwenye mashindano ya kimataifa. Tangu kuajiriwa kwa Barbara Gonzalez kama afisa mtendaji mkuu wa timu, Wekundu hao wa Msimbazi wamekuwa wakifanya vyema sana kwenye mechi zao.

Ujio wa Kocha mpya, Didier Gomez, timu imekuwa ikifanya vyema sana na kufanikiwa katika mechi zote za nyumbani na hata ugenini. Didier Alikuja na mbinu mbalimbali ambazo zimekubalika na wachezaji na hata mashabiki wa Msimbazi. Ilifanikiwa kushinda goli moja dhidi ya AS Vita ugenini na kumfunga bingwa wa Afrika Al Ahly uwanja wa Mkapa.

Simba

Mwanzoni mwa msimu Barbara alidai kuwa malengo ya klabu msimu huu ni kufika nusu fainali ya kombe la mabingwa Afrika, lakini kutokana na uchezaji wao, watu wengi wanaamini wanaweza kufika Fainali kabisa.

Katika VPL, timu hii inashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 46 na michezo minne mkononi. Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara, alisema timu hii kubwa Afrika itachukua kombe la VPL kwa mara nyingine tena. Kwa hiyo mashabiki wa timu hiyo wanamatuamini makubwa sana na kuchukua makombe mengi zaidi.

Kupatikana kwa mchambuzi wa video na vifaa maalum vya kupima uchezaji wa timu, umeaminika kuleta mafanikio makubwa kwa msimbazi. Katika hatua ya Makundi, Simba walifanikiwa kutoa angalau wachezaji wawili katika kila mechi ya timu bora ya wiki ya Afrika. Wachezaji wao wawili pia, Luis Miquisonne na Clatous Chama walitajwa kama wachezaji bora wa wiki mara mbili.

Simba sasa imerejea VPL, na wataendelea ligi hiyo huku wakisubiri kujua timu itakayokumbana nae katika michuano ya kimataifa, huku droo ikitegemewa kupigwa tarehe 30 mwezi huu.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

simba, Simba Ni “Next Level” Sasa, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa