Klabu ya wanawake ya Simba Queens imeendeleza rekodi ya ubabe mbele ya Yanga Princess kwa msimu wao wa nne mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa jana Uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

 

simba queens, Simba Queens Wababe Dabi ya Kariakoo., Meridianbet

Simba Queens imeweka rekodi ya kushinda mechi sita kati ya saba ilizowahi kukutana na Yanga Queens kwenye ligi. msimu wa 2018/19, Simba Queens ilishinda mabao 7-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza kisha mabao 5-1 kwenye mzunguko wapili

Msimu wa 2019/20 waliendeleza ubabe kwa kushinda mabao 3-1 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza kabla ya mzunguko wapili kushinda mabao 5-1.

Msimu uliopita mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga iliambulia sare ya bila kufungana kule Mo Bunju Arena kabla ya kufungwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa mzunguko wapili.

Ushindi huo umeifanya Simba kurudi kileleni kwenye msimamo wa ligi na kuishusha Fountain Gate ambayo ilikuwa inaongoza kwa alama tisa wakati Simba baada ya kushinda imekusanya alama 11.

Mabao ya Simba Queens yalifungwa na Oppah Clement aliyefunga mawili pamoja na Asha Djafar ambaye pia alifunga mawili huku bao pekee Yanga likufungwa na Aisha Masaka kwa mkwaju wa penalti.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa