Maneno hayo yamesemwa na Nahodha wa timu ya Simba SC John Bocco katika mkutano wa waandishi wa habari juu ya mchezo wa kimataifa kuelekea robo fainali za kombe la Africa CAF, mchezo huo utakaochezwa kati ya Simba SC dhidi ya AS Vita Club katika uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa, kesho tarehe 3 Aprili, saa 10 kamili Alasiri.

“Kwa upande wetu kama wachezaji tuko vizuri, tuna ari nzuri ya kuweza kupambana ili kufikia malengo ya timu yetu. Tumefanya maandalizi mazuri na tunaamini Mungu atatusaidia na tutafuzu hatua ya robo fainali.

Nahodha wa Timu ya Simba SC - John Bocco Akizungumza na waandishi wa habari
Nahodha wa Timu ya Simba SC – John Bocco Akizungumza na waandishi wa habari

“Tuna wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaoelewa kwanini wapo kwenye klabu. Tuko tayari.”– Alisema Nahodha wa klabu ya simba John Bocco.

Simba

“Kesho ni lazima tupate matokeo ili tusonge mbele, tumejipanga kupata matokeo. Tunamshukuru Mungu hakuna mchezaji ambaye tutamkosa, wote wapo kambini na hilo linatupa mwanga kuwa tunaweza kufanya vizuri.”- Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Selemani Matola akizungumza kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya AS Vita Club.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

simba, Simba SC: Tupo Vizuri na Tayari Kupambana – Bocco, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

  1. Nawakubari simba najuwa mpotiyali kwalolote sisi mashabiki tunasubili point 3 tuuu mungu yupo pamoja nanyi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa