Nyota na nahodha wa klabu ya Simba Sports Club John Raphael Bocco inaelezwa kuna uwezekano mkubwa akatolewa kwa mkopo katika klabu ya Ihefu kutoka jijini Mbeya.

Klabu hiyo iliopanda ligi kuu msimu na kutwaa ubingwa wa ligi daraja la kwanza baada ya kushuka daraja msimu wa 2020/21 wameonesha nia ya kumuhitaji nyota huyo wa klabu ya Simba aliecheza mafanikio makubwa katika ligi kuu ya Tanzania Bara.

Bocco, Bocco kutolewa kwa Mkopo Ihefu., Meridianbet

Ihefu pia inaelezwa wapo katika ushindani mkubwa na klabu ya Singida Big Stars ambao pia wanamuwania nyota huyo. Inaripotiwa klabu ya Ihefu ipo tayari kumlipa staa huyo mshahara anaopewa ndani ya klabu ya simba. mazungumzo yakienda vizuri basi John Bocco atajiunga na Ihefu Fc kutoka jijini Mbeya.

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Azam siku za hivi karibuni amekua akikosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama mara kwa mara.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa