WAKIJIANDAA na mchezo wa ligi dhidi ya Simba, timu ya KMC imerejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambao utapigwa Septemba 7 mwaka huu.

Kikosi cha KMC ambacho kilikuwa jijini Arusha kwa ajili ya mechi mbili za Ligi dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union kimeambulia pointi moja.

Simba, KMC Yarejea Kambini Kuiwinda Simba, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa: “Timu ilirejea Dar Jumatatu na kutoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji ambapo jana Jumanne kiliingia kambini na kuanza kwa program ya gym na leo hii asubuhi kuendelea na mazoezi ya kawaida ya uwanjani.

“Katika kipindi hiki cha mapumziko tutakuwa na program mbalimbali ikiwemo kucheza mechi za kirafiki ambapo kesho tutakuwa ugenini dhidi ya As Arta Solar 7 kutoka nchini Djibout mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru, Dar.

“Kwa kipindi hiki ambacho tupo kwenye mapumziko, tunahitaji mechi nyingi za kirafiki kadri ambavyo tutazipata, na tayari tumepata mechi moja ambayo tutacheza kesho lengo ni kufanya maboresho ambayo yataiwezesha Timu kufanya vizuri zaidi katika michezo inayokuja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa