Kiungo nyota wa klabu ya simba Mzamiru Yassin leo amesaini kandarasi mpya itakayomuweka kwenye viunga vya msimbazi kwa miaka miwili zaidi kuichezea klabu hiyo hadi mwaka 2024.

Mzamiru yassin alijiunga na klabu ya Simba mwaka 2016, akitokea klabu ya walima miwa wa Morogoro Mtimbwa Sugar, ambayo  inashiriki ligi kuu ya Tanzania bara.

Mzamiru, Mzamiru Amwaga Wino Simba Hadi 2024, Meridianbet

Mzamiru Yassin amezaliwa mwaka 1996, na mchezo wake wa kwanza wa kimataifa kwenye timu ya taifa ya Tanzania ulikuwa ni mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Zimbabwe, ambapo tanzania walishinda 3-0.

Kwa sasa tetesi zote ambazo zilikuwa zinamhusu kiungo huyu zimemalizwa, Mzamiru ni nyekunde nyeupe mpaka 2024.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa