Kiungo wa Kimataifa wa Ghana Augustine Okrah ambaye jana alitambulishwa na Simba kuwa mchezaji mpya wa timu hiyo amesema anataka kufanya vitu vingi vikubwa kwenye timu hiyo, lakini muhimu taji la ligi kuu, kufika mbali kimataifa na kuwa msaada kwa timu.

Okrah alisema hayo kwenye utambulisho wake akiwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano w Simba Ahmed Ally, ambapo kubwa alisisitiza anataka kutizimiza kila lengo la klabu hiyo kwenye msimu unaokuja na yupo tayari kuipambania timu.

Okrah

Akizungumzia juu ya ujio wake ndani ya Simba Okrah alifunguka: “Najua Simba ni timu kubwa Afrika na ina matumaini makubwa sana kwangu ndiyo maana wamenisajili, nina hamu ya kufanya makubwa kwenye timu hii.

“Lakini jambo la kwanza ni kurejesha ubingwa wa ligi na kufanya vizuri kwenye mashindano ya ndani, kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na mimi kuwa mchezaji tegemea na mwenye msaada mkubwa kwa timu hii.”

Okrah amekuwa mchezaji wa tatu wa kigeni kutambulishwa ndani ya Simba, alianza Moses Phiri kutoka Zambia na Victor Akpan raia wa Nigeria ambaye alikuwa anacheza Coastal Union.

Wengine ambao wamesajiliwa na Simba ni Watanzania, Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza akiwa mshambuliaji na Nasoro Kapama aliyekuwa akisukuma gozi kwenye kikosi cha Kagera Sugar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa