LEO alhamis wachezaji wa Simba na benchi la ufundi wameondoka kuelekea mji wa Ismailia nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki tatu ya kujiandaa na msimu ujao.

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa “Tutakuwa na makundi matatu ambapo kundi la kwanza ndio tunaondoka leo (jana) wengine visa zao zimechelewa, huku wengine wakiwa na timu zao za taifa.

Simba, Simba Asepa Dar kibabe, Meridianbet

“Ndani ya wiki hii tutacheza mechi ya kirafiki kutokana na mipango ya kocha na programu zake ambazo nimeziona.

“Ligi itakuwa ngumu na msimu ujao itakuwa zaidi, niwapongeze viongozi wetu kwani tumepata wachezaji tuliowahitaji kwa msimu huu.

“Muhilu ana matatizo kidogo na baada ya siku mbili tutajua anapoelekea kwani kwa sasa anaendelea na mazungumzo na viongozi.”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa