Simba SC wanaendelea kushusha vifaa kwani leo jumatatu wamemtambulisha rasmi kiungo wao kutoka Kagera Sugar, Nassoro Kapama.

Kapama kwa msimu uliopita chini ya Kocha Mkuu wa kikosi cha Kagera, Francis Baraza amefanikiwa kucheza mechi 18 na kutoa asisti moja.

Simba

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba imeeleza kuwa “Kipaji kikubwa kutoka kwenye ardhi iliyobarikiwa ya Tanzania kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu.”

Usajili huo kwa Simba unakuwa wa nne mpaka sasa, huku kayi yao wawii wakiwa wachezaji wa kigeni na wawili wazawa wakisajiri. Victor Akpan akitokea nchini Nigeria, Moses Phiri akitokea nchini zambia, Habib Kyombo na Nassoro Kapama wote ni wazawa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa