WACHEZAJI na benchi la ufundi la klabu ya Simba, wanatarajia kuanza safari ya kurejea Dar kesho jumatano wakitokea Mji wa Ismailia, nchini Misri walipoweka kambi.

Simba waliweka kambi huko yakiwa ni maandalizi ya msimu ujao wa ligi ambapo wanatarajia pia kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika.

Simba, Simba Kutua Dar kesho, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kikosi hicho kitarejea nchini na kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa tamasha la Simba Day.

“Kikosi kimeendelea kujiweka fiti leo baada ya kucheza mechi tatu za kirafiki na wanatarajia kuanza safari ya kurejea Dar kesho jumatano na siku ya alhamis mchana kitakuwa kimewasili tayari.

“Wachezaji wote wapo fiti pia kuhusu suala la wale wachezaji waliorudi Dar kwa ajili ya mazungumzo na klabu akiwemo Meddie Kagere, Chris Mugalu na Thadeo Lwanga likimalizika tutaweka hadharani.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa