Simba vs Yanga Ulinzi Kuimarisha Zaidi Agosti 13

Dar Dabi, polisi wajizatiti kuiamaraisha ulinzi zaidi kwenye mchezo wa mahasimu wa kariakoo ambao ni Simba yenye makazi mtaa wa msimbazi na Yanga yenye makazi mtaa wa twiga kwenye mchezo wa ngao ya jamii siku ya Jumamosi Agosti 13.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar kwa ajili ya ufunguzi wa ligi kwa msimu wa 2022/23.

Akizungumzia hilo, Kamanda, Jumanne Muliro amesema kuwa: “Tumejipanga kuimarisha ulinzi kabla, wakati na baada ya mchezo.Β 

“Jeshi la Polisi linatoa tahadhari na onyo kwa wale wote watakaoingia na silaha kwenye mchezo huo isipokuwa wale wenye mamlaka ya kuingia nazo.Β 

“Wajiepushe na fujo msiende na matokeo mfukoni kwani hatutavumilia kwa wanaofanya vurugu, hivyo mchezo utakuwa salama watu wajitokeze.”

Acha ujumbe