Klabu ya Simba imepangwa kuvaana na timu kutoka Malawi Nyasa Big Bullets kwenye hatua ya awali ya michuano Ligi ya Mabingwa Afrika lakini uongozi wa Simba umesama kuwa hawana presha kwani tayari walishajipanga kukutana na klabu yoyote huku wakiweza kuwa kocha zoran tayari ameanza kufanya tathmini ya ubora na mapungufu ya Wamalawi

Juzi Jumatano kwenye makao makuu ya Shirikisho la soka Afrika (CAF), ilifanyika droo ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo Simba walipangiwa kucheza na Nyasa Big Bullets ya Malawi huku watani zao wa jadi Yanga wakianza na Zalan ya Sudani Kusini.

Simba, Simba Wakabidhiwa Wamalawi CAF, Meridianbet

Katika hatua hiyo ya awali inayotarajiwa kuanza kuchezwa Septemba 9, mwaka huu Simba itaanzia ugenini kabla ya kucheza mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye uwanja wa, Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Septemba 16, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema: “Tumepokea vizuri matokeo ya droo iliyofanyika jana (juzi), Jumanne na achana na Nyasa Big Bullets, sisi tumeshafanya maandalizi yote ya ndani na nje ya uwanja na tulikuwa tayari kucheza dhidi ya timu yoyote ambayo tungepangwa dhidi yao.

“Tayari benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Zoran limeanza kufanya tathimini ya wapinzani wetu na tuna matumaini makubwa ya kufikia malengo yetu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa