Kocha Mkuu wa Simba Zoran Maki ameweka wazi kuwa anaamini kwamba watapata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga kutokana na maandalizi na hana hofu na mechi hiyo.

Maki ambaye ni mrithi wa mikoba ya Pablo Franco aliyefungashiwa virago Mei 31, mwaka huu, kete yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Yanga, Agosti 13 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba
SIMBA SC

Maki alisema kuwa anatambua kuhusu ratiba ilivyo na mechi kubwa ambazo atakutana nazo ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Yanga.

“Kikubwa ni kuheshimu kila mchezo, najua kwamba kuna Dabi hilo lipo wazi na hata ambapo nilikuwa kulikuwa na jambo kama hili hivyo sina mashaka na mchezo wetu dhidi ya Yanga kikubwa ni maandalizi mazuri.” Alisema Maki.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa