Simba Yatozwa Faini Ya Milioni 15 Na TPLB Kutokana Na Vurugu Za Mashabiki

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeitoza klabu ya Simba SC jumla ya Sh. 15,000,000 kutokana na makosa mawili ya mashabiki wake, yaliyotokea katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Young Africans, ambapo Simba ilishinda 2-1.

Simba Yatozwa Faini Ya Milioni 15 Na TPLB Kutokana Na Vurugu Za MashabikiUamuzi huo ulifikiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya TPLB katika kikao chake cha Oktoba 21, 2026, kilichopitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi. Kwa mujibu wa taarifa ya bodi hiyo, Simba imetozwa faini ya Sh. 10,000,000 kwa mashabiki wake kurusha chupa uwanjani zaidi ya mara moja wakati mchezo ukiendelea.

Simba Yatozwa Faini Ya Milioni 15 Na TPLB Kutokana Na Vurugu Za MashabikiBodi imeeleza kuwa hili ni kosa la kujirudia kwa mashabiki wa Simba ndani ya msimu wa 2026/2027, kwani mashabiki hao walifanya kosa kama hilo katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 48:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Simba Yatozwa Faini Ya Milioni 15 Na TPLB Kutokana Na Vurugu Za MashabikiAidha, Simba imetozwa faini nyingine ya Sh. 5,000,000 kutokana na mashabiki wake kuvamia eneo la kuchezea wakati mchezo unaendelea, ambapo mmoja wao alimfuata kijana mwokota mpira (ball kid) na kumfanyia fujo. Tukio hilo lilidhibitiwa na walinzi wa uwanja. Adhabu hii nayo imetolewa chini ya Kanuni ya 48:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.