Simba Wanataka Makombe Yote Msimu Huu

UONGOZI wa Simba ni kama umewatumia ujumbe mzito watani zao wa jadi Yanga baada ya kuweka wazi kuwa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2022/23 umejipanga kuhakikikisha unarudisha makombe yao yote ambayo waliyapoteza msimu uliopita.

Simba msimu uliopita walipoteza Kombe la Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam Sports na taji la Ngao ya Jamii ambapo mataji hayo yote yalichukuliwa na wapinzani wao wakubwa Yanga.

Matchday : Orlando Pirates vs Simba SC.

Kuelekea tamasha lao la wiki ya Simba litakalofanyika Agosti8, mwaka huu, Uongozi wa timu hiyo jana Jumanne uliungana na mashabiki wao kutoa msaada kwa kituo cha kutunzia wazee, Kigamboni Dar es Salaam.

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Simba, Barbara Gonzalez alisema: “Tunajua Wanasimba wanataka nini na nikuhakikishie kuwa msimu huu hatutarudia makosa ambapo tumejipanga kuhakikisha tunarudisha makombe yote ambayo tuliyapoteza msimu uliopita na kwa mipango tuliyonayo bila shaka tutafanikiwa.

Naye Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Tumejipanga na naweza kusema tupo tayari kwa ajili ya msimu ujao, malengo makubwa ya Simba ni katika kuhakikisha tunafanya vizuri katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na katika hili tumejipanga kufanya ukatili mkubwa wa dakika 90.”

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi maalum, Amon Mpanju ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo alisema: “Tunawashukuru Simba kwa kujali watu waliosahaulika, hii ni sawa na ibada. Katika maadhimisho yenu pia ni muhimu kuhusisha ujumbe wa kupambana na ukatili kwa jamii.”

Acha ujumbe