Klabu ya Simba SC iliyo na maskani yake mitaa ya Msimbazi imeondolewa rasmi katika mashindano ya klabu bingwa Afrika baada kushindwa kufunga magoli manne hapo jana dhidi ya Kaizer Chiefs.

Simba sc ilikuwa na wakati mzuri sana katika kilichoaminika ni kwenda kupindua meza kibabe, wanamsimbazi walitakiwa kushinda magoli matano ili waweze kuvuka na kuingia nusu fainali ya klabu bingwa Afrika.

Katika mechi iliyokuwa imelala upande mmoja, huku Simba wakishambulia na kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa, ilishuhudia nahodha wa timu hiyo akiingia kambani mara mbili huku Chama akimalizia goli la 3.

Mchezo ulianza kwa vijana wa Gomez kuonesha nia ya kushinda mechi hii huku wakipeleka mashambulizi mengi langoni mwa Kaizer bila mafanikio mpaka pale dakika ya 23 ambako John Bocco alitupia goli maridhawa kabisa, huku wakipoteza nafasi nyingi mno za kufunga magoli katika mechi hii.

Katika mechi hiyo pia, kocha alimtoa Mzamiru Yasin na kumuingiza Morrison ambaye alileta mabadiliko sana katika mchezo huo huku akiwatesa sana mabeki wa The Amakhos. Mechi ilishuhudia pia Onyango na Lwanga wakitolewa kutokana na majeraha ya vichwa waliyopata baada ya kugongana.

Kutokwa kwao kuliingiza Kenned Juma na Erasto Nyoni ambao walituliza Simba kwa kiwango kizuri sana na kufanya timu yao ishambulie bila wasiwasi, kimsingi wana wa Telanga walikuwa kwenye siku yao.

Hata baada ya mchezo huo mashabiki wa timu hii walionekana kuridhika na kiwango kizuri cha timu yao licha ya kuondolewa kwenye michuano hiyo. Bingwa huyu mtetezi wa VPL ameshinda mechi 7, kapoteza 3 na kutoka sare 2 katika michezo yote 12 ya mashindano haya.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa