Timu ya Simba imefanikiwa kuendelea kujikita kileleni mwa VPL baada ya hapo jana kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji pale kwa Mkapa.

Katika mechi ya jana, Simba walionekana kutawala magoli kwa muda wote huku wakifanikiwa kushinda goli moja tu kipindi cha kwanza kutoka kwa Mugalu kutokana na Dodoma Jiji kukaba nafasi za kati ya uwanja kwa kiwango kikubwa.

Mshambuliaji Chris Mugalu aliwapa simba bao la kwanza dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Rally Bwalya. Dakika ya 29 Dodoma ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Cleophas Mkandala kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Anuari Jabir uliomponyoka mlinda mlango Aishi Manula.

Luis Miquissone alitupatia bao la pili dakika ya 55 baada ya kumalizia pasi iliyopigwa kiufundi na Clatous Chama.

Mugalu aliongeza bao la tatu dakika ya 67 kwa shuti kali la chini chini akiwa ndani ya 18 kufuatia kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Chama.

Kocha Didier Gomez aliwatoa Mzamiru Yassin, Miquissone na Mugalu na kuwaingiza Bernard Morrison, Ibrahim Ajibu na Medie Kagere. Mabadiliko yaliyoonekana kuongeza sana mashambulizi langoni mwa Dodoma Jiji.

Baada ya Mechi Gomez alieleza kufurahishwa sana mchezo mzuri wa timu yake na kujikita kileleni kwa alama nyingi zaidi ndio lengo kuu.

Kutokana na matokeo ya mechi hiyo, Simba sasa ipo kileleni ikiwa na alama 61 huku watani wao wa jadi Yanga wakiwa na alama 55 na michezo miwili zaidi ya Simba. Mechi ijayo ya Simba ni dhidi ya Yanga tarehe 8 mwezi ujao!

Kwao wao wanasemaje kuhusu mechi hiyo?


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa