Timu ya Simba SC imepanda nafasi 15 kutoka nafasi ya 28 mpaka nafasi ya 13 kwa viwango vya vilabu barani Afrika.

Timu hii yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi imefanikiwa kufika nafasi hiyo baada ya michezo yake ya viwango vya juu kabisa katika michuano ya klabu bingwa Afrika mwaka huu!

Simba imefanikiwa kupanda viwango hivyo baada ya kuongezeka alama kadhaa na sasa kuwa na jumla ya alama 399 nyuma tu ya Enyimba Aba ya Nigeria yenye alama 408. Endapo timu hii itafanya poa na kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Klabu bingwa Afrika basi itaongeza alama zaidi na nafasi yake itapanda zaidi.

Kutokana na mabingwa hao wa Tanzania kufanikisha kujikusanyia alama hizi, sasa Tanzania imefanikiwa kuwa miongoni mwa Nchi zitakazotoa timu nne kwenye mashindano ya CAF, yaani timu mbili kwenye klabu bingwa na timu mbili kwenye shirikisho!

Kongole kwa Msimbazi na Kongole kwa Tanzania kwa hatua kubwa hii na bila shaka sasa ni wakati wa Tanzania kutambulika kisoka duniani kote bila ya kupepesa macho!


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa