Azpilicueta Atangaza Kustaafu Soka Mwisho wa Msimu

Beki wa zamani wa Chelsea FC, César Azpilicueta, ametangaza rasmi kuwa atastaafu soka la ushindani mwishoni mwa msimu huu baada ya kucheza kwa zaidi ya miaka 20 katika kiwango cha juu.

Azpilicueta Atangaza Kustaafu Soka Mwisho wa MsimuAzpilicueta, ambaye kwa sasa anaitumikia Sevilla FC, alithibitisha taarifa hiyo kupitia ujumbe wa hisia alioutoa Ijumaa asubuhi, akieleza kuwa ulikuwa wakati mgumu kwake kuandika barua ya kuaga mchezo huo alioupenda maisha yake yote.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Leo nataka kushiriki nanyi kwamba msimu huu utakuwa wa mwisho kwangu kama mchezaji wa kulipwa. Baada ya miaka mingi ya kuishi ndoto yangu, nahisi umefika wakati wa kuanza ukurasa mpya wa maisha yangu,” alisema Azpilicueta.

Azpilicueta Atangaza Kustaafu Soka Mwisho wa MsimuNyota huyo mwenye umri wa miaka 36 alisema hakuwahi kufikiria kuwa angekuwa na safari kubwa kiasi hicho tangu alipokuwa mtoto akicheza mpira mjini Pamplona nchini Spain. Pia aliwashukuru watu wote waliokuwa sehemu ya mafanikio yake ndani na nje ya uwanja.

Azpilicueta Atangaza Kustaafu Soka Mwisho wa MsimuKatika kipindi chake cha miaka 11 ndani ya Chelsea, Azpilicueta alicheza zaidi ya mechi 500 na kushinda mataji makubwa tisa, jambo lililomfanya kubaki kuwa mmoja wa wachezaji wenye heshima kubwa katika historia ya klabu hiyo ya London Magharibi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.