Kiungo mkongwe James Milner ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 40, akihitimisha safari ya miaka 24 katika Ligi Kuu England Premier League yenye mafanikio makubwa. Milner amekuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza kwa muda mrefu zaidi katika historia ya ligi hiyo.
Milner alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Leeds United kabla ya kuichezea Newcastle United, Aston Villa, Manchester City, Liverpool na klabu yake ya mwisho Brighton & Hove Albion. Katika kipindi hicho, ameweka rekodi ya kucheza mechi 658 za Premier League na kushinda mataji makubwa ikiwemo mataji matatu ya ligi, FA Cups mbili, EFL Cups mbili na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika ujumbe wake wa kuaga kupitia mitandao ya kijamii, Milner alisema “Baada ya misimu 24 katika Premier League, nahisi huu ndio wakati sahihi wa kumaliza safari yangu ya uchezaji soka wa kulipwa.” Aliongeza kuwa mashabiki wote waliomuunga mkono wamekuwa sehemu muhimu ya mafanikio yake.
“Kwa mashabiki, asanteni kwa kila kitu. Msaada wenu umekuwa na maana kubwa zaidi kuliko mnavyoweza kufikiria. Hata wale waliokuwa wakinikosoa, asanteni pia kwa sababu mmenifanya niwe mchezaji bora na mtu bora,” alisema Milner katika ujumbe wake wa kuaga.
Alitoa pia shukrani kwa familia yake akisema “Kwa familia yangu, asanteni kwa kila kujitolea, kila safari na kila moyo wa kunitia nguvu. Bila ninyi haya yote yasingewezekana.” Alisisitiza kuwa anaondoka kwenye soka akiwa na fahari kubwa na kumbukumbu zisizofutika.
Milner alihitimisha kwa kusema kuwa soka limempa zaidi ya alivyowahi kufikiria, akiwashukuru wote waliokuwa sehemu ya safari yake ndefu ya mafanikio katika kandanda ya England na Ulaya.


