Rio Ferdinand Awasili Tanzania Kwa Ziara Maalum ya Siku Nne

Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand, amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku nne ambapo amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wadau wa michezo. Miongoni mwa waliompokea ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.

Rio Ferdinand Awasili Tanzania Kwa Ziara Maalum ya Siku NneMamia ya mashabiki walijitokeza katika eneo la mapokezi la uwanja huo kwa ajili ya kumpokea gwiji huyo wa soka aliyewahi kung’ara katika kikosi cha Manchester United chini ya kocha maarufu Alex Ferguson. Ujio wake umeibua hamasa kubwa kwa mashabiki wa soka nchini kutokana na historia yake kubwa ndani ya mchezo huo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Ferdinand alijiunga na Manchester United mwaka 2002 akitokea klabu ya Leeds United na kufanikiwa kuwa sehemu ya kikosi kilichotawala soka la England pamoja na Ulaya kwa miaka kadhaa. Katika kipindi chake Old Trafford, alitwaa mataji mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2008.

Rio Ferdinand Awasili Tanzania Kwa Ziara Maalum ya Siku NneBaada ya kustaafu soka, Ferdinand ameendelea kubaki karibu na mchezo huo kupitia kazi ya uchambuzi na utengenezaji wa maudhui ya michezo, ambapo hufanya mahojiano na wachezaji na makocha kutoka sehemu mbalimbali duniani. Umaarufu wake umeendelea kuvutia mashabiki wengi wa kandanda duniani kote.

Rio Ferdinand Awasili Tanzania Kwa Ziara Maalum ya Siku NneUjio wa nyota huyo nchini Tanzania unaelezwa kuwa fursa muhimu katika kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia michezo na utalii. Ziara yake pia inatarajiwa kuongeza hamasa kwa vijana wanaofuatilia soka pamoja na kuimarisha mahusiano ya michezo kati ya Tanzania na mataifa mengine.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.