KAMATI ya uendeshaji na usimamizi wa ligi maarufu kama kamati ya masaa 72 imeibakiza timu ya African Sports kwenye michuano ya Championship kwa msimu ujao.

Mchezo wa mtoano wa marudiano kati ya African Sports dhidi ya Rhino Rangers uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ulivunjika kutokana na mwamuzi wa pembeni kurushiwa jiwe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamati hiyo leo jumamosi imeeleza kuwa timu ya African Sports imepewa ushindi wa mabao matatu na pointi tatu hivyo wataendelea kubaki katika michuano hiyo.

“Timu ya African Sports imepewa alama tatu na mabao matatu huku Rhino Rangers ikipoteza mchezo huo kwa kosa la kuvuruga mchezo huo hadi kusababisha kuvunjika.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa