MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amefunguka juu ya timu yake ya Simba pamoja na wachezaji wake kukosekana kwenye tuzo za Afrika ambazo Yanga wapo na kuwepo kwenye tuzo za NBC za mwezi uliopita na kusema kuna vitu havikuwa sawa kwa tuzo za mwezi.
Ahmed Ally alisema wao kutokuwepo kwenye vinyang’anyiro vya tuzo za CAF, kwa sababuz zile zinahusu msimu uliopita na wao kama Simba wanazungumza vitu ambavyo vinahusu msimu huu.Kuhusu Balake kukosa Tuzo ya Mchezaji Bora Mwezi Septemba ambayo ilikwenda kwa Wazir Junior wa KMC alisema: “Kuhusu swala la tuzo za wachezaji wa Simba kutopata tuzo za wachezaji bora kwenye ligi au kutoonekana kwenye tuzo za timu bora ya mwaka kule CAF ngoja nikujibu kwa hoja.
“Sitaki kukosea heshima lakini kuna ule mwezi Wazir Junior alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi, kwenye taarifa kuliandikwa amekuwa mchezaji bora sababu amefunga mabao mawili, wakati Jean Baleke alifunga mabao matatu.
“Ni maajabu kuona aliyefunga mabao matatu kwa mwezi mzima amechukua tuzo mbele ya mtu aliyefunga mabao, yaani wa mabao matatu ni bora kuliko wa mabao matatu, inashangaza kidogo.“Kuhusu swala la tuzo za CAF, hizo ni tuzo za msimu uliopita, nipo hapa kuzungumza kuhusu Simba ya msimu huu,” alisema Ahmed Ally.