Ahmed Ally Amaliza Utata Inshu ya Kanoute

Sadio Kanoute ni moja ya viungo wenye msaada mkubwa sana pale kwenye klabu ya Simba SC, akisaidizana vyma kabisa na kiungo mwenzake fahari ya Morogoro zao la Mtibwa Sugar Mzamiru Yassin. Kwa haraka haraka unaweza kusema Kanoute na Mzamiru ni roho ya Simba huku ubongo wa Simba akiwa ni Clatous Chama.

 

simba

 

Knaoute amekuwa akifaya kazi ngumu na chafu sana haswa pale kwenye eneo la kati, kitu ambacho kinapelekea kuonywa kwa mdomo na waamuzi na muda mwingine kwa kanuni ya kadi ya njano kama ambavyo kwenye mechi ya jana kati ya Coastal Union alivyoadhibiwa kwa kadi ya njano na kufanya kuwa na kadi mbili za njano.

Kikanuni ni nini hatma ya Kanoute kwenye michezo inayofuata?

Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally amefafanua utata wa tukio hilo kwa kunukuu kifungu cha kanuni za Mpira wa Miguu kwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

“Katika Mchezo dhidi ya Coastal, Sadio Kanoute alioneshwa kadi ya pili ya njano iliyopelekea kwa mujibu wa Kanuni kupewa kadi nyekundu.

 

simba

Ufafanuzi wa Kanuni ya 41(2.1)

“Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kadi mbili za njano (second yellow card) katika mchezo wa ligi hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuata wa timu yake.

“Hivyo basi Kanoute atatumikia adhabu katika mchezo unaofuta ambao ni Kombe la Azam Sports dhidi ya EAGLE utaochezwa 10/12/2022 Jijini Dsm” Aliandika Ahmed Ally kwenye Instagram akaunti yake.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Acha ujumbe