AHMED ALLY: AL AHLY TUNAWAMUDU NA TUTAKOMAA NAO

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya kikosi cha Simba amebainisha kwamba watakwenda na kasi ya wapinzani wao Al Ahly Waarabu wa Misri kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali.

Ikiwa imeweka kambi Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali nguvu kubwa kwa Simba ni kupata matokeo kwenye mchezo wa kwanza utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.ahmed allyMachi 29 Simba wanatarajiwa kushuka uwanjani na Machi 30 Yanga nao watakuwa na kibarua dhidi ya Mamelodi Sundowns mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 kwa wababe hao.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa wanatambua kwamba ushindani ni mkubwa lakini watakwenda sawa na wapinzani wao kupata matokeo chanya.

“Wanasema Al Ahly wakifika hatua hii huwa wanabadilika nasi tunasema wakibadilika tunabadilika nao malengo ni nikuona kwamba tunafika hatua ya nusu fainali safari hii” Alisema Ahmed Ally.ahmed ally“Hii ni Simba timu yenye wachezaji wazuri, watu wa mpira lakini wapinzani wetu wanatuchukulia kawaida, sasa niwaambie ukweli kwamba makali yetu yapo palepale kupoteza mchezo ama kutoshinda mabao mengi haina maana kwamba hatuna ubora.

“Taratibu kila mechi kunakuwa na mabadiliko na unaona kabisa mpira unapigwa na wachezaji makini kikubwa ni kuona tunaendelea kuwa imara na kupata matokeo kwenye mechi zetu zote, tunahitaji kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na tunaamini kwamba tutapata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Al Ahly,”.

Acha ujumbe