Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa tuzo ya mashabiki bora ambayo wamepata kutokana na kushiriki michuano ya African Football League ni heshima kubwa kwao.

 

AHMED ALLY ANATAMBA NA TUZO YA AFL

Ikumbukwe kwamba Simba iligotea hatua ya robo fainali kwa kuondolewa na Al Ahly ya Misri. Baada ya kutwaa tuzo hiyo walibainisha kuwa ni ya kila shabiki wa Simba.


Jana Novemba 12 Simba walikabidhiwa tuzo hiyo Afrika Kusini katika fainali ya pili iliyochezwa Uwanja wa Loftus Versfeld ambapo mabingwa wa michuano hiyo mipya waliibuka kuwa ni Mamelod mbele ya Wydad Casablanca.

Ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Muhene, (Try Again) alikabidhiwa tuzo hiyo.

AHMED ALLY ANATAMBA NA TUZO YA AFL

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa jambo hilo ni kubwa na linaleta heshima

Try again amesema: “Tuzo hii ni kwa kila shabiki wa Simba. Kuja kwenu uwanjani kushangilia timu yenu kumeiwezesha timu yetu kushinda Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL. Pongezi nyingi kwenu.,”

AHMED ALLY ANATAMBA NA TUZO YA AFL
Kwa upande wa Ahmed Ally amesema haya kuhusu tuzo hiyo: “Tumeshinda tuzo ya mashabiki bora wa Afrika

Hongereni sana wana Simba mnastahili heshima hii, mmeonesha tofauti ya mashabiki wa mpira na wanywa Supu za vibudu. Alisema msemaji huyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa