Afisa Habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally amewashauri mashabiki wa klabu hiyo kuamka na kuangalia michezo ijayo ya timu hiyo na kusahau haraka kipigo cha bao moja kwa bila walichokipata mchezo uliopita kutoka kwa Azam FC.

 

Ahmed Ally: "Lazima Tuamke Tuangalie Yajayo".

Ahmed ameyasema hayo, hapo jana wakati timu yake ikijiandaa kumenyana dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho majira ya saa 1:00 usiku.

Simba mpaka sasa yupo nafasi ya 3 na ameshacheza mechi 7 kwenye ligi kuu na ameshinda mechi 4 kapata sare 2 na kapoteza mchezo mmoja akiwa na pointi 14, Wakati kwa upande wa Mtibwa yeye yupo nafasi ya 2, baada ya kucheza michezo 9, ameshinda mechi 4, sare 3 na amepoteza mara 2.

Ahmed Ally: "Lazima Tuamke Tuangalie Yajayo".

Mechi 10 za mwisho kukutana kwenye Ligi, Simba ameshinda mara 6, Wameenda sare michezo minne huku Mtibwa akishindwa kufurukuta mbele ya Mnyama. Vilevile Ahmed amewasihi wananchi kujitokeza hapo kesho kuja kuishuhudia timu yao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa