Afisa habari na mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe ameshushiwa rungu na bodi ya ligi kuu ya Tanzania baada ya kuonekana kumkejeli mwamuzi Tatu Malogo.
Ali Kamwe amepigwa faini ya shilingi milioni moja na bodi ya ligi akituhumiwa kumkejeli mwamuzi Tatu Malogo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram baada ya mchezo baina ya klabu ya Simba na Singida Fountain Gate.Baada ya mchezo baina ya klabu ya Singida Fountain Gate waliokua nyumbani kuikaribisha klabu ya Simba msemaji huyo alipandisha chapisho lenye picha ya mwamuzi Tatu Malogo likisindikizwa na maneno yaliokua yakisomeka kama “Maokoto”.
Bodi ya ligi imetafsiri kua Afisa habari huyo alimaanisha kua mwamuzi huyo alipokea hongo kwakua neno “Maokoto” kwa maana isiyo rasmi inamaanisha hela hivo kamati imetafsiri kusudio la msemaji huyo wa klabu ya Yanga lilikua ni kumkejeli mwamuzi huyo.Chapisho la Ali Kamwe lilipelekewa kwa kiasi kikubwa na maamuzi yaliyotolewa katika mchezo huo ambayo yalikua yana utata na yakionekana kuipendelea Simba, Hivo Afisa habari huyo ndio akachapisha chapisho ambalo limemueka matatani.