Ali Kamwe: Malengo Yetu Kubeba Ubingwa wa Afrika

Afisa Habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema malengo yao makubwa msimu huu ni kubeba kombe la Afrika ambalo wanashiriki kwasasa ambalo ni kombe la shirikisho Afrika.

Msemaji huyo amefunguka kua malengo yao msimu huu sio kufika hatua fulani kwenye kombe la Afrika na lengo mama la mabingwa hao wa kuhistoria ni kubeba kombe la Afrika ndani ya msimu huu licha kukosekana kwa muda mrefu.ali kamweKlabu ya Yanga ambayo imeingia hatua ya makundi kombe la shirikisho mwaka 2017 kabla ya mwaka huu, Hivo klabu ya Yanga kupitia msemaji wake inaamini uwezo wanao wa kubeba ubingwa huo wa Afrika.

Ali Kamwe bila kusahau amezungumzia wapinzani wao kwenye kundi lao ambao klabu yake imepangwa nao akisema ni timu nzuri na bora ndo maana zimefika hatua ambayo zipo, Huku akizungumzia zaidi klabu ya Tp Mazembe ambayo wameshakua mabingwa mara kadhaa wa michuano hiyo na akisema hiyo inaonesha ugumu wa kundi lakini lengo ni kubeba taji hilo.ali kamweAfisa habari Ali Kamwe pia hakuacha kuzungumzia suala la usajili kuelekea dirisha dogo mwezi Januari huku akisema klabu hiyo itafanya usajili kutokana na matakwa ya benchi la ufundi la klabu hiyo na si vinginevyo.

Acha ujumbe