Ally Shaban Kamwe, Afisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga Sc amesema kuwa watu hawataki kusema ukweli kuwa wapo baadhi ya wachezaji wao wanaanza kwenye kikosi cha Mamelody Sundowns.
Kamwe amemiminika Kwa kusema; “Hii ni fact na mchambuzi anayeweza aje tufungue mjadala.“Ingekuwa miaka ya zamani Wachezaji wetu wa Yanga Sc kuingia kikosi cha Mamelodi Sundowns ilikuwa shida ila kwa Yanga Sc hii Wachezaji 6 mpaka 7 wanaanza kwenye kikosi cha Mamelodi Sundowns.
“Wachambuzi chambueni mnavyoweza, na Mchambuzi anayeweza aje hapa tufungue Mjadala, taja wako nitaje Wangu. Huu mchezo tunautaka na tumenuwia Kushinda,” alisema ALI KAMWE