OFISA Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa kiungo wa timu hiyo AZIZI KI hawezi kucheza timu nyingine yoyote nchi hii isipokuwa Yanga.
Ali Kamwe, aliweka wazi kuwa ni kweli kuwa nyota huyo ambaye ni Moja kati ya vinara wa mabao nchi hii yupo kwenye nyakati za mwisho za mkataba wake.“Aziz Ki ni kweli anamaliza mkataba wake lakini kwa hapa sioni kama kuna timu ambayo Aziz anaweza kucheza, Aziz Ki anahitajika na timu nyingi kwa hizi timu za Afrika Kusini Aziz hawezi kucheza na watu wanaofanya dhuluma namna ile.
“Ziko ofa nyingi lakini kubwa ambalo naweza kuwaambia wanayanga, wachezaji bora ambao wamewaona kwenye kikosi chetu wanasalia kwenye kikosi chetu.”Alisema Ali Kamwe.