MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Hassan Dalali na Msanii Mkubwa Afrika Ali Kiba walikutana kwenye uzinduzi wa Simba Day Morogoro, ambapo safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiendelea. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Mzee Dalali amesema miongoni mwa mambo ambayo anatamani kuona ni Mkoa wa Morogoro una uwanja mkubwa na wenye hadhi ya kimataifa ili timu hiyo ihamie hapo.
Mzee Dalali amesema hayo katika stendi ya zamani mjini humo muda mfupi baada ya msafara wa Simba kuwasili ukitokea Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua wiki ya Simba Day ikiwa ni pamoja na kutambulisha jezi za msimu ujao wa 2024/25 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi zinakaribia kuanza, usije kupishana na gari la Mshahara.
Mwanzilishi huyo wa Simba Day amesema Morogoro timu yao iliwahi kutangaza ubingwa mara mbili wakati akiwa kiongozi, hivyo ina historia nzuri na mkoa huo.
“Mjenge uwanja sasa Simba ibakie hapa Morogoro. Hapa ni nyumbani kwetu japo Simba ni ya kila sehemu. Leo tunazindua jezi, nawaomba wana Simba kila mmoja akanunue jezi tuujaze uwanja tukiwa na jezi zetu. Tofauti na zamani mwaka huu jezi zimetoka kabla ya Simba Day,” amesema Mzee Dalali.
“Jezi za awamu hii ni hatari tu kudadadeki… jamaa (Yanga) nawapa salamu. Mimi ndio mwanzilishi wa Simba Day ila tarehe 8 siku yetu halisi tunakutana na wale jamaa kazi wanayo. Tuna wachezaji hawalogeki. Tunaanza tarehe 3 katika siku yetu kabla ya wale mabwana nao kuona chamoto,” amesema Mzee Dalali.
KIBA AITEKA MORO
Msanii wa Bongofleva, Alikiba ametambukishwa na Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally mjini Morogoro kuwa ndiye mtumbuizaji kinara katika tamasha la 16 la Simba Day kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Semaji la CAF, kama ambavyo amekuwa akipenda kujiita Ahmed, alimtangaza Kiba akisema: “Mabibi na mabwana, nasema hivi Alikiba ndiye atakayetumbuiza Simba Day.”
Mara baada ya kutambulishwa Kiba alipanda jukwaa kuu akiwa na usaidizi wa mabaunsa na kuwasalimia mashabiki wa Simba ambao wamejitokeza katika stendi hiyo ya zamani.
Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.