Bodi ya Ligi Kuu nchini imemtangaza mwamuzi wa kimataifa, Ahmed Arajiga kuwa ndiye atazisimamia sheria 17 za soka katika mchezo wa NBC Premier League kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC.
Arajiga atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga, Kassim Mpanga wa Dar es Salaam huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Tatu Malogo.
Kariakoo Derby itachezwa Jumamosi ya Aprili 20, 2024 saa 11:00 jioni.