AUCHO, PACOME, YAO KUWAKABILI MAMELODI

NYOTA watatu wa Yanga ambao walikosena kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mamelody Pacome Zouzoua, Khalid Aucho na Yao Attahoula wanatarajia kuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mechi ya marudiano.

Msemaji wa Yanga Ali Kamwe amesema, timu hiyo inakwenda Sauz ikiwa imetimia tofauti na ambavyo ilikuwa wiki iliyopita wakitoka Suluhu na Mamelodi wakiwa Dar.aucho“Tunakwenda Sauz tukiwa tumetimia haswa Kwa Sasa, wachezaji wetu ambao walikosena kwenye mechi iliyopita Tunakwenda nao ambao ni Khalid Aucho, Pacome, Attouhla Koussi Yao.

“Wamefanya mazoezi na wenzao na Kwa Uwezo wa Mungu watakuwepo Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano,”alisema Ali Kamwe.

Acha ujumbe