Breaking News: Aucho, Pacome Zouzoua Wapo Tayari| Yanga vs Mamelodi

VIUNGO tegemezi wa Yanga SC, Khalid Aucho na Pacome Zouzoua watakuwepo kwenye mechi ya mkondo wa kwanza kati ya Yanga na Mamelody March 30, Baada ya majeraha Yao kuendelea vizuri. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

pacome

Hayo yamesemwa na Ali Kamwe ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo.

Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Kamwe alisema: “Tumeingia kwenye wiki ya mechi yetu na Mamelodi Sundowns, Khalid Aucho yupo fit asilimia 70, maana yake wiki hii ataanza mazoezi ya uwanjani.

“Shomar Kibwana leo ataanza mazoezi, tayari yupo sawa. Zawad Mauya yeye tayari alishaanza mazoezi.

“Kuhusu Pacome Zouzoua watu wote ni mashahidi juzi walimuona akiwa kwenye benchi wakati Ivory Coast ikicheza dhidi ya Benin. Mchezaji akikaa benchi maana yake yupo kwenye mpango wa kocha.

“Kwa hiyo kama alikuwa kwenye mpango wa mwalimu maana yeke yupo fit ndio maana alikaa kwenye benchi. Ni habari njema ambayo viongozi, wanachama na wapenzi wa Yanga tumeifurahia.

“Yao ndio mchezaji pekee ambaye kucheza mechi dhidi ya Mamelodi Sundowns bado ni 50/50, huyu tusubiri.”

Beti na Meridianbet mechi hii kali kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Acha ujumbe