kiungo Mshambuliaji wa Azam FC, Awesu Awesu amejiunga na klabu ya KMC kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Azam Awesu sasa amesajiriwa rasmi na klabu ya KMC ambayo aliitumikia kwa mkopo na kufanikiwa kuonesha kiwango kikubwa kwenye kikosi hicho.

Awesu, Awesu Aajifunga Mmoja KMC, Meridianbet

Awesu ambaye alisajiriwa na klabu ya Azam akitokea klabu ya Mtibwa Sugar, wakati akiwa kwenye kikosi cha Azam FC kiungo huyo hakufanikiwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa chini ya kocha Lwandamina na kupelekwa kwa mkopo kwenye kikosi cha KMC.

 

Akizungumzia usajili huo, Awesu amesema kuwa “Mkataba wangu na Azam umemalizika lakini tayari nimesaini mkataba wa mwaka mmoja na KMC.

“Ni changamoto mpya kwangu lakini hiyo hainipi shida kwani nimecheza kwa msimu uliopita hivyo nitaendelea kupambana.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa