KOCHA wa Klabu ya Azam FC Kally Ongala ametaja kile kinachisumbua timu yake kwa kushindwa kuwa na makali katika eneo la ushambuliaji na hivyo kupoteza umakini na ufanisi wa kupata magoli zaidi.

Azam FC ilipata ushindi kwa tatu dhidi ya Coastal Union wa mabao 3-0 goli la ushindi wakifunga dakika za nyongeza, baada ya kipa wa Coastal Union kuonekana kupoteza muda kwa makusudi.
Ongala alisema kuwa wachezaji waliaowaanzisha mbele hakuwa na muunganiko mzuri.
“Tulianza chini kidogo wenzetu walijitahidi, makosa tulifanya wenyewe wakapata bao la kusawazisha lakini baadae tukapata matokeo, watu tuliowaanzisha mbele chemistry yao haikuwa nzuri, tatizo kubwa tukipoteza mpira timu inakuwa haina mpangilio, lakini tunayarekebisha hayo”.

Kwa upande wa kocha mkuu wa timu ya Coastal Union Yusuf Chipo alielezea matokeo hayo yanatokana na kitu gani kwenye timu yake huku akijivunia timu yake kuifunga Azam magoli mawili.
“Tunafungwa mabao ambayo tunafanya makosa kwenye safu ya ulinzi, kufunga tunafunga, tumeifunga Azam mabao mawili, nani alishawahi kuifunga? sisi tumeifunga” Alifafanua Chipo.
Kwa ushindi huo unaifanya Azam kufikisha alama 32 na yupo nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga SC ambao wana magoli mengi zaidi ya kufunga wakiwa na mabao 23 na wamefungwa 6 huku Azam akiwa na mabao 21 ya kufunga na 13 ya kufungwa.
Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.


