Azam FC wanajipanga kusaka alama tatu kesho Jumatano kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza dhidi ya Singida Big Stars, wakati ambao Singida na wao wanataka kufufukia kwenye mgongo wa Azam FC.
Singida hawajashinda mechi yoyote kati ya mechi zao tatu za Ligi Kuu ambazo wamecheza hivi karibuni. Walichapwa gemu mbili na kutoka sare kwenye mechi Moja.Kocha Mkuu wa Azam FC Yusuph Dabo, ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwenye mchezo wao dhidi ya Singida ni kupata alama tatu, Kwa kuwa na wao watumie amekuwa na Mwendo wa kusuasua .
Walikosa alama tatu mbele ya Tabora United pamoja na mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons ambapo ilishindikana kutokana na ushindani kuwa mkubwa