KOCHA Mkuu wa Azam FC, Kali Ongala ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Azam Sports Federation leo dhidi ya Malimao.

Huu ni mchezo wa raundi ya Pili ambapo Mwana Chamazi atakuwa mwenyeji kwenye mchezo wa leo Desemba 9 2022 unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Ongala amebainisha kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wanatambua ugumu uliopo hivyo wataingia kwa nidhamu.

Azam Fc Kuyakamua Malimao Chamazi

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Malimao ambao ni wa Kombe la Shirikisho, maandalizi yamekamilika na tunatambua kwamba ushindani utakuwa mkubwa,”.

Miongoni mwa wachezaji wa Azam FC ambao walikuwa sehemu ya kikosi kilichofanya maandalizi ya mwisho ni pamoja na kiungo Tepsi Evance.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa