Azam FC na Dodoma Jiji Mechi ya Kibabe Leo

Kombe la Shirikisho la Azam kuendelea hii leo ambapo Matajiri wa Chamazi Azam FC watamenyana na Dodoma Jiji majira ya saa 1:00 usiku katika Dimba la Chamazi Complex.

 

Azam FC na Dodoma Jiji Mechi ya Kibabe Leo

Azam ambayo ipo chini ya kocha Kally Ongala wametoka kupoteza mchezo wao uliopita kwenye ligi wakiwa ugenini huku matarajio ya kutetea taji la ligi kuu ya Tanzania yakiyeyuka kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri kwenye mechi zao.

Wakati kwa upande wa Dodoma Jiji nao wakiwa bado wanatafuta njia ya kutoka katika nafasi waliyopo wametoka kupoteza mechi yao ya ligi iliyopita wakiwa nyumbani licha ya kuahidiwa pesa endapo wangeshinda mechi hiyo.

Azam FC na Dodoma Jiji Mechi ya Kibabe Leo

Na sasa timu hizi zinakutana katika Kombe la FA huku kila timu ikitazamia kufanya vizuri hii leo. Tofauti ya pointi kati ya timu hizi mbili ni 22, huku mechi ya mwisho kukutana Wanalamba lamba waliondoka kifua mbele.

Je hii leo Dodoma watakubali kuendelea kuwa wateja wa Kally Ongala kwani toka mechi tano za mwisho hawajawahi kupata ushindi zaidi ya kuambulia sare pekee.

Acha ujumbe