AZAM FC NAO WAMPIGA MTU MKONO

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wanaingia kàtika orodha ya timu ambazo zimepata ushindi mkubwa katika mechi za Azam Sports Federation ikiwa ni raundi ya tatu.

Ubao wa Uwanja wa Azam Complex Februari 22, 2024 baada ya dakika 90 ilikuwa Azam FC 5-0 Green Warriors.AZAM FCMabao ya Idd Suleiman Nado dakika ya 32, Kipre Junior dakika ya 33, Paul Kyabo dakika ya 56 alijifunga, Abdul Sopu dakika ya 65 na Ayoub Lyanga dakika ya 83.

Azam FC itakutana na Mtibwa Sugar iliyopata ushindi wa mabao 3-2 Stand United katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu.

JKT Tanzania 5-1 TMA Stars inaingia kwenye orodha ya timu zilizopata ushindi mkubwa hivi karibuni huku mabingwa watetezi Yanga nao walipata ushindi wa mabao 5-0 Polisi Tanzania.AZAM FC

Ushindi huo unaifanya kuingia anga za Yanga ambayo ilipata ushindi kama huo kwenye mchezo wao uliopita uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Acha ujumbe