AZAM FC WANA JAMBO LAO KIMATAIFA

UONGOZI wa Azam FC umebainisha kuwa kwenye anga la kimataifa wanaimani watafanya kitu kikubwa ambacho kitawashangaza wengi ambao hawana imani na timu hiyo.

Ipo wazi kwamba Azam FC itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa baada ya kugotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 69.azam fcHasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa kila kitu kipo kwenye mpango bora na walikuwa wanahitaji kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tulianza msimu kwa mpango kazi kutokana na kile ambacho kilikuwa kwetu na wengi hawakutarajia kwamba tutakuwa hapa na imetokea kwa kuwa tunakwenda kimataifa tutafanya kitu.azam fc“Mpango wa mwanzo ilikuwa kufanya vizuri kwenye ligi ya ndani imekuwa hivyo na sasa tunakwenda kwenye anga la kimataifa tutafanya vizuri kwa kuwa mipango ipo vizuri.”

Acha ujumbe