Azam Fc Wanaitaka Ngao ya Jamii

UONGOZI wa Azam FC umebainisha kuwa utaanza na Ngao ya Jamii kwenye ufunguzi wa msimu wa 2023/24.

Yanga na Azam zinatarajiwa kumenyana Agosti 9 Uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni hatua ya nusu fainali.Azam FcOfisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa wapo tayari kwa msimu mpya na wataanza na Yanga.

“Mchezo wetu wa kwanza wa ushindani msimu mpya ni dhidi ya Yanga katika Ngao ya Jamii tupo tayari kwa ajili ya ushindani na wachezaji wapo tayari.

“Kikukubwa ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo wetu na wapinzani wetu tunawaheshimu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema Ibwe.Azam FcAzam FC kambi yake kwa maandalizi ya msimu wa 2023/24 ilikuwa ni Tunisia na Yanga kambi yao ipo AVIC Town, Kigamboni.
Tayari imerejea Dar na kuanza mazoezi Uwanja wa Azam Complex ikiwa na maingizo mapya na miongoni mwao ni Yannick Bangala aliyekuwa Yanga sawa na Feisal Salum.

Acha ujumbe